Hivi zile kokoto pembeni ya reli zinasaidia nini?

Ujue nishawahi fikiria hichi kitu kitambo kidogo, ila leo ngoja niulize haya. 

Hivi zile kokoto pembeni ya reli zinasaidia nini?

Freshman Asked on November 10, 2018 in Elimu.
Add Comment
2 Answer(s)

Kwa kawaida njia ya treni hutengenezwa kwa kufunga pau mbili za feleji sambamba kwenye boriti za mbao, simiti au chuma zinazokaa juu ya msingi wa mawe ya kokoto.

Kazi za kokoto kwenye msingi wa reli ni nyingi, ila mojawapo ya kazi kuu ni  pamoja na

  • Kuwezesha upenyeshaji wa maji, njia ya treni ama reli ni adui mkubwa wa maji hivyo ili kuifanya reli ikae mahali pasipo na utuamaji wa maji kokoto husaidia pia kokoto hizo huzuia mimea iliyo chini ya reli kuchomoza juu na kuwa kama kizuizi
  • Kazi nyingine ni kuwashikilia pau mbili za reli ambazo ndio njia ya treni.  Hivyo treni ikipita ipite bila pau hizo kuteleza ama kuhama njia yake
Junior Answered on November 22, 2018.
Add Comment

Ni kweli kwamba mawe ya relini yanafanya kazi nyingi. Kwanza kabisa, yanasaidia reli kukaa mahali pake wakati treni yenye uzito mkubwa ikiwa inapita. Pia inazuia aina yoyote ya majani yasiote karibu na reli ambayo yanaweza kuufanya udongo uliopo chini ya reli kuwa dhaifu na kushindwa kuhimili uzito wa reli na treni.

Kazi nyingine muhimu inayofanywa na mawe ya relini ni kuzuia maji yasikusanyike au kukaa muda mrefu kwenye reli na kudhoofisha njia ya reli. Hiyo haimaanishi kuwa mawe hayo yanaingika njia ya reli dhidi ya maji kwa asilimia 100, la hasha! Haiwezekani lakini inawezesha mifereji ya maji chini na kuzunguka kwenye njia ili maji hayo yasikae muda mrefu na kudhoofisha uthabiti wa reli.
Kwa maelezo zaidi tembelea https://www.google.com/amp/www.fikrapevu.com/kwanini-kuna-mawe-madogo-madogo-kwenye-reli/amp/

Senior Answered on July 23, 2019.
Add Comment

Your Answer

By posting your answer, you agree to the privacy policy and terms of service.