Je, Binadamu anaweza ishi sayari ya Mars?

NASA kutoka Marekani waliweza fika mwezini kabla ya nchi yeyote ile duniani, sasa naona shauku imehamia Mars, kuna nini cha kuvutia sana Mars? na Je, binadamu anaweza ishi? au anahitaji nini ili apate kuishi?

Sophomore Asked on December 8, 2018 in Space.
Add Comment
1 Answer(s)

Inaonekana kama kila mtu anawaza Mars siku hizi. NASA inataka kutuma binadamu kwenye sayari hiyo nyekundu kufikia mwaka 2030, na SpaceX (Chini ya Elon Musk) inataka kufika huko mapema zaidi, ina mipango ya kuwa na watu kufikia mwaka 2024.

Mars ni mandhari maarufu kwa Hollywood, filamu kama The Martian na filamu ya Life ya mwaka 2017 zinaonyesha tuu nini ambacho tunaweza ona mara baada ya kufika sayari hiyo jirani, lakini filamu hizi hazijibu swali moja muhimu – mara tu binadamu akifika huko, jinsi gani ataweza kuishi muda mrefu?

Anga ya Mars ina kiwango kikubwa sana cha kaboni dioksidi, uso wa sayari ya Mars ni baridi sana kuendeleza maisha ya binadamu, na gravity ya sayari hiyo ni 38% tu ya Dunia. Pia, anga ya Mars ni sawa na asilimia 1 ya anga ya dunia katika usawa wa bahari. Hiyo inafanya safari ya kuingia sayari ya Mars kuwa ngumu. NASA itafikaje huko? Tunawezaje kutumaini kukabiliana na hali hiyo?

RE: Je, Binadamu anaweza ishi sayari ya Mars?

Mars ina rasilimali zote zinazohitajika ili kuendeleza maisha ya binadamu. chuma, Carbon, Maji barafu, Silicon, na karibu kila element inayohitajika kusaidia maisha Duniani inaweza kupatikana katika aina mbalimbali hata Mars. Kutumia rasilimali hizi, tunaweza kutengeneza plastiki, metali, vifaa vya umeme, ambavyo tunaweza tumia kutengenza nguo, makazi, magari, kompyuta, paneli za jua, waya, mabomba, vyombo, au kitu kingine chochote tunachohitaji.

Kwa muda mfupi, inawezekana kuzalisha oksijeni na mafuta ya roketi (Methalox) huko Mars kwa kutumia Reaction Sabatier inayojulikana, ambayo hutumia hidrojeni na kaboni dioksaidi inayopatikana kwa wingi katika mazingira ya sayari hiyo  kuzalisha Methane na maji, ambayo inaweza vunjwa vunjwa kwa njia ya electrolysis kuzalisha oksijeni kwa upumuaji na Hydrogeni ya kutumia kama mafuta

Katika uzalishaji wa chakula, majaribio yamefanyika kukuza ngano, beats, karoti, na mazao mengine mengi katika udongo uliotengenezwa hapa duniani kwa kufananisha na ule unaopatikana sayari ya Mars, jaribio limeonyesha mafanikio. Hata hivyo inajulikana kuwa udongo wa Mars hauna nitrojeni ya kutosha, pia kutokana na anga kua nyembamba yenye mwanga hafifu wa jua inaweza kuwa kitu kigumu kukuza mimea kwa ajili ya madawa na chakula.

Kwa bahati nzuri wanasayansi kutoka  Eindhoven University of Technology, huko Netherlands wamegundua majani bandia (artificial leaves). Majani hayo, yaliundwa kwa mpira wa silicone, yanaweza kubadilisha mwanga mdogo wa jua kuwa nishati ya kutosha kusababisha chemical reactions katika uzalishaji wa madawa na kompaundi zinginezo.

RE: Je, Binadamu anaweza ishi sayari ya Mars?

Professional Answered on December 9, 2018.
Add Comment

Your Answer

By posting your answer, you agree to the privacy policy and terms of service.