Je tumefeli wapi hadi hakuna wasanii toka East Africa katika Album ya #THEGIFT ya Beyonce?

Album ya mwanadada Beyonce imeachiwa, hivi karibuni akiwa ameshirkiana na wasanii toka Ghana, Nigeria na South Africa. Album hiyo ni kwaajili ya soundtrack katika movie ya The Lion King. Utayarishaji wa movie hiyo umetumia maeneo mengi ya East Afrika kama Serengeti na Kilimanjaro, huku pia kukiwa na wimbo maarumu kwaajili ya Serengeti. Pia wimbo wa Spirit umetumia maneno ya kiswahili. Lakini kwanini hakuna msanii hata mmoja toka East Africa?

Senior Asked on July 21, 2019 in music.
Add Comment
2 Answer(s)

The Gift ina nyimbo 14, ndani ya albamu wasanii toka marekani kama Childish Gambino, Pharrell Williams na Kendrick Lamar wameshirikishwa na pia kuna wasanii toka Afrika magharibi na kusini walioshirikishwa. Upo sahihi, Afrika mashariki hatujatokea katika albamu hiyo iliyosubiriwa kwa hamu sana .

Sababu za sisi kutoshirikishwa ni nyingi, lakini la msingi ni kujiuliza kuwa wasanii wetu wanafanya mziki wao wawe maarufu Instagram na kuonekana FIESTA tu au wanafanya kujitambulisha na kujitangaza ndani na nje ya nchi?Wasanii wetu hawapo tayari kuingia katika soko la kimataifa ndio maana wameridhika na soko la ndani.

Kabla sijaanza kujibu swali lako emb tambua kuwa kitu kinachomtofautisha msanii wa Tanzania na msanii wa nchi zingine kama Nigeria na Afrika kusini ni utamaduni, wasanii wa Tanzania hawauishi utamaduni wao kama nchi hizo. Alama pekee ya kuonekana ya kumtambulisha Msanii wa Tanzania haipo, zaidi ya Kiswahili ambacho hakionekani. Emb mtazame msanii kama Mr Eazi, tazama anavyovaa, tazama anavyoongea, sikiliza sauti ake afu njoo Tanzania, nani wa kumlinganisha nae? Mpoto? au nani?

 

Kufikia hapo unagundua kuwa, mziki wa bongo bado haujaingia soko la kimataifa. Vitu vingi hukwamisha mfano, katika media rushwa hutembezwa ili msanii fulani asikike, vikwazo vingine huletwa na mifumo mibovu ya benki zetu ambazo hufanya mihamala ya kimataifa kuwa migumu na mlolongo mrefu , mfano mzuri wasanii wanapata shida kujiunga na platform kubwa kama Spotify na iTunes kiurahisi kama ilivyo nchi zingine.

Kikwazo kingine ni kuwa, wasanii wengi wachanga wa bongo hawaji na sauti zao ila wanakaa kuiga na kurudia sauti na miziki ya nje na Nigeria, kwa kufanya hivyo wanahisi wanavuti mashabiki wa nje, La Hasha.

 

Freshman Answered on July 21, 2019.
Add Comment

Ukweli uko wazi kabisa kwamba East Africa mfano mzuri ni hapa kwetu.. tuna washairi na si wanamuziki kwa sababu ndogo tu kwamba tuko hodari kuandika lakini bila kufuata kanuni na guidlines za wanamuziki…unakuta mtu anajiita mwanamuziki lakini hawezi kupiga hata filimbi sasa huo sio muziki hayo ni mashairi muziki unatengenezewa na computers,,,sasa ndo hapo msanii wa East Africa ukisikiliza audio yake na live ni kama kaiba au sio yeye….

Senior Answered on July 22, 2019.

Man umetisha aisee

on July 23, 2019.
Add Comment

Your Answer

By posting your answer, you agree to the privacy policy and terms of service.