Jinsi gani naweza angamiza Kunguni(Bed bugs) nyumbani?

Jinsi gani naweza angamiza Kunguni(Bed bugs) nyumbani?

Rafiki yangu amekuwa akiwashwa mwili mzima  hasa wakati wa usiku, baada ya kufanya utafiti Google nikagundua ana  vipele aina ya hives  (Urticaria) . Tumekuja gundua vipele hivyo anapata kutokana na kutembewa na  kunguni. Sasa tunahitaji msaada wa jinsi gani tunaweza angamiza wadudu hawa

Professional Asked on November 9, 2018 in afya.
Add Comment
5 Answer(s)
Best answer

Katikati ya karne ya 20, wanadamu walihisi wamefaulu kuwaangamiza kunguni. Mimi binafsi nimewafahamu wadudu hawa kupitia ule usemi wa : “Don’t let the bed bugs bite you.”

Ripoti moja ya mwaka wa 2012 kuhusu kuwadhibiti wadudu hao inasema: “Katika miaka 12 ambayo imepita kunguni wameanza kuonekana tena nchini Marekani, Kanada, Mashariki ya Kati, nchi kadhaa za Ulaya, Australia, na katika sehemu fulani za Afrika.”

Watu fulani hubeba kunguni bila kujua wanapoenda dukani, kwenye kumbi za sinema, au hotelini. “Upende usipende utabeba kunguni,” anasema meneja fulani wa hoteli nchini Marekani. “Maadamu hoteli inapata wateja lazima kunguni wataendelea kuwapo.” Kwa nini ni vigumu kiasi hicho kuwamaliza kunguni? Unaweza kujilindaje? Kunguni wanapovamia nyumba yako, unaweza kuchukua hatua gani zinazofaa ili kuwaondoa na kuwazuia wasirudi tena?

Wadudu Wasiokufa kwa Urahisi

Kwa kuwa wadudu hao ni wadogo kama mbegu ya tofaa na wana mwili bapa, kunguni wanaweza kujificha mahali popote pale. Wanaweza kujificha katika godoro lako, fanicha zako, sehemu ya ukutani ya kuunganishia vitu vya umeme, au hata kwenye simu yako. Kwa kawaida kunguni hupenda kujificha mita tatu hadi sita kutoka kwenye vitanda na maeneo ya kuketi. Kwa nini? Ili wawe karibu na chakula chao, yaani, wewe!*

Mara nyingi, kunguni huwauma watu wanapolala. Hata hivyo, watu wengi hawahisi wanapoumwa kwa sababu mdudu huyo humdunga mtu kitu kinachogandisha kinachomwezesha kuendelea kula kwa dakika kumi hivi bila kukatizwa. Na ingawa kunguni wanaweza kula kila juma, imesemekana kwamba wanaweza kuendelea kuishi bila kula kwa miezi mingi.

Tofauti na mbu na wadudu wengine, inaonekana kwamba kunguni hawaenezi magonjwa ya kuambukiza. Hata hivyo, wanapomuuma mtu wanatokeza mwasho na baadaye sehemu hiyo inavimba, na watu wengi huathiriwa kihisia. Watu walioumwa na kunguni wanaweza kupoteza usingizi, kuaibika, na hata kufikiri kwamba kunguni amewauma muda mrefu baada ya wadudu hao kutoweka. Jarida moja nchini Sierra Leone linasema kuwa kunguni “ni wasumbufu sana na wanawakosesha watu usingizi” na linaonya kuhusu “aibu inayohusianishwa na kunguni.”

Kuwadhibiti Kunguni

Kunguni wanaweza kumsumbua mtu yeyote. Ni rahisi kuwadhibiti ukitambua mapema kwamba wapo. Kwa hiyo, jifunze kutambua ishara za kwamba wapo nyumbani na unaposafiri. Chunguza fanicha zako na vitu vingine vya mbao pamoja na mizigo, uone ikiwa kuna mayai madogo yanayofanana na mbegu ndogo nyeusi au alama za damu. Tumia tochi unapowatafuta kunguni ili uweze kuwaona.

Usiruhusu kunguni wawe na sehemu nyingi za kujificha. Ziba nyufa zote ukutani na kwenye viunzi vya milango. Ingawa kunguni hawaletwi na uchafu, itakuwa rahisi zaidi kuwatambua na kuwadhibiti ikiwa unasafisha nyumba kwa ukawaida na kupunguza vitu vilivyorundamana. Ukiwa hotelini, unaweza kupunguza uwezekano wa kubeba kunguni kwa kuepuka kuweka masanduku yako sakafuni na kitandani.

Source: wol.jw.org

Sophomore Answered on November 9, 2018.
Add Comment

Kufikia dakika hii, binafsi nafahamu kuna dawa nyingi zinauzwa madukani lakini  nafahamu ukichanganya sabuni ya unga,mafuta ya taa na chumvi unakuwa umetengeza sumu ya kuua wadudu wengi akiwemo mdudu kunguni.

Mafuta ya taa  yana uwezo wa kuua wadudu wengi kama kunguni na pia  mafuta hayo huwafukuzia mbali wadudu. Lakini hakuna ushahidi kama mafuta ya taa yanweza anagamiza hata mayai yao.

Kibaiolojia,  mayai ya kunguni (bed bugs) yana ukuta mnene hivyo upenyaji wa sumu ni mgumu sana. Mda pekee wa  kuwapata wadudu hawa ni pale baada ya kutoka kwenye mayai.

Jamani, natoa tahadhari kwa yeyote yule atakayetumia mafuta ya taa katika zoezi hili, mafuta ya taa yanaweza sababisha moto hivyo ukaishia kuchoma nyumba yako. Hivyo kuwa makini

Sophomore Answered on November 14, 2018.
Add Comment

apo kuna njia hizi
1.tengeneza mchanganyiko wa chumvi.. sabuni ya unga.. na mafuta ya taa kisha spray kwenye godoro
2.au nunua dawa kwa wanaotembeza

Junior Answered on July 18, 2019.
Add Comment

Binafc nishanunua dawa japo nimeisahau kidogo ila ni ya kufanania na dawa nyingine kwa jina la (lava) dawa hiyo ukiispray mfano leo utaendelea kuwaona kunguni ndani ya wiki nzima ila baada ya hapo wanapotea kabisa
Ni mwaka wa nne sasa sina kunguni

Sophomore Answered on August 29, 2019.
Add Comment

Bwana huyu mdudu ni mjeuri sana na anatengeneza mayai mengiiiii hatari hata ukiwauwa wote mayai yakabaki baada ya mwezi hali inarudi kama kawaida, na hata akibaki mmjoa tu usipo muua basi ni kazi bure…..me naona solution ni kuchoma godoro tu na kununua jipya wale wadudu hawafai

Senior Answered on July 25, 2019.
Add Comment

Your Answer

By posting your answer, you agree to the privacy policy and terms of service.