kipi kilianza kati ya yai na kuku??

Bible

Add Comment
2 Answer(s)

Kulingana na jibu alilotoa James Chungu katika swali hili,

Kwa muda mrefu wengi tumekuwa tukidhani kuwa yai ndilo lililoanza kabla ya kuku lakini kutokana na ushahidi wa kisayansi kama alivyosema Dakta Colin Freeman kutoka Chuo Kikuu cha Sheffield aliyeshirikiana na watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Warwick. Watafiti hao wa Kiingereza wanasema kuwa kuku ndiye aliyeanza kabla ya yai kwa vile yai linaweza kupatikana tu kwa chembechembe za protini ziitwazo ovocledidin-17 (OC-17) zinazopatikana katika mifuko ya uzazi ya kuku
Protini hiyo inayofanya kazi kama kichocheo (catalyst) kuharakisha maendeleo ya yai, ilitambuliwa kabla na ilihusishwa na uzalishaji wa yai lakini kwa kuchunguza kwa undani wanasayansi hao wakagundua namna gani protini hiyo inavyowezesha hatua hiyo (ya kutengeneza yai).
Wanasayansi hao walitumia kompyuta yenye uwezo wa hali ya juu (supercomputer) ifahamikayo kama HECToR,ambayo ipo jijini Edinburgh,Scotland, kukuza (zoom) hatua zinazoonyesha jinsi yai linavyozalioshwa.Ilibainika kuwa OC-17 ni muhimu katika kuanzisha kukomaa (crystallization)-hatua ya awali katika uundwaji wa gamba la yai.Protini hiyo hugeuza calcium carbonate kuwa chembechembe za calcium (calcite crystals) ambazo ndizo zinazounda gamba la yai,huku zikitengeneza gramu 6 za gamba katika kila masaa 24.
Ukiachana na utafiti huo,Kama wewe ni Muumini wa Dini utakumbuka kwenye vitabu kuwa Mungu aliumba Kiumbe na Akaamrisha Vizaliane Hakuumba Yai ili limzae kuku. Ila aliumba Kuku na Yai lipo Kwenye mzunguko wa maisha yake.
Sophomore Answered on March 20, 2020.
Add Comment

Apo inafaamika mkuu kuku ndo ilianza Ni Sawa na kuuliza Kati ya binadamu na sperm Nini kilianza

Freshman Answered on March 11, 2020.
Add Comment

Your Answer

By posting your answer, you agree to the privacy policy and terms of service.