Kufikiri sana na kupoteza nywele kichwani kuna uhusiano gani?

Answered

TUMESIKIA mtu anapofikiri sana inapelekea kupoteza nywele kichwani. Je sababu au muunganiko wa vitu hivi viwili ni nini?

Senior Asked on July 19, 2019 in sayansi.
Add Comment
1 Answer(s)
Best answer

Hakuna uhusiano kati ya kupoteza nywele na kufikiria sana,sema kuna mambo ambayo yanaweza yakasababisha nywele kupotea..
1.infections kama fungal infection (fangasi mba) zinaweza zikasababisha nywele kudhoofu na kuleta muwasho kwenye ngozi ya kichwa (scalp) na katika kujikuna hupelekea kupotea kwa nywele ambazo zinaweza zisirudi…
2. Supply ya damu katika scalp ipo sana kuzunguka kichwa (parietal, temporal na occipital) na hafifu juu ya scalp kitu kinachosababisha mtu anavyoongezeka miaka supply kuzidi kua hafifu na hupelekea nywele kukos nutrients za kutosha na kupotea..
3. Kijenetikia (genetic inheritance) pia ni sababu kama kwenye familia kuna watu wenye vipara hakika kuna chance kubwa ya watu wengine pia kupata upotevu wa nywele katika familia hiyo…
4.umri mkubwa pia ni tatizo mifumo mingi inaleta shida hivyo hata nywele si ajabu kupotea…
NB:
Kupoteza nywele na kufikiri sana hakuna uhusiano wowote kwani mbona Daktari ben carson ni mtu mashuhuri mwenye kufikiri sana lakini hana kipara..

RE: Kufikiri sana na kupoteza nywele kichwani  kuna uhusiano gani?


Eistein mwenyewe mwanasayansi mwenye IQ kubwa yakufikiri lakini kipara kikowapi labda cha kutafuta😎

RE: Kufikiri sana na kupoteza nywele kichwani  kuna uhusiano gani?

Senior Answered on July 26, 2019.
Add Comment

Your Answer

By posting your answer, you agree to the privacy policy and terms of service.