kwanini wengi tunaamini yesu ni mweupe na shetani ni mweusi???

Answered

hii imani nadhani watu wengi wanayo leo hii uone picha ya mtu mweusi na uambiwe kua ni yesu ndhani itakua ni vigumu kdg kuamini

Junior Asked on July 29, 2019 in religion.
Add Comment
2 Answer(s)
Best answer

Watu wanaamini ivyo kwa sababu mambo mema hufanywa kwenye mwanga na maovu daima hufanywa gizani ,,,hivyo basi kwa sababu Yesu ni Mungu na hana dhambi na ndio maana anafananishwa na kuwa mweupe asie na doa na shetani anafananishwa na weusi kama mkaa yaani ndio baba wa dhambi…
Na si kwamba yesu ni mzungu eti kwa maana hakuna mtu leo mwenye ushahid kwani haya yote ni mapokeo tu kutoka kwenye biblia ambayo hata yenyewe haijataja rangi ya yesu…
Na juzi juzi apa kumetokea hoja mbalimbali kua yesu alikua mkushi(mweusi) wa egypt …na watu hao wanasababu zao huwezi kuwapinga…
Pia yesu imezieleka kuwa ni mzungu kwa sababu walioandika biblia (kwamsaada wa Mungu) na waliotuletea dini hii ni wazungu hivyo sidhani kama jngekua rahisi kwao kumuweka Yesu mweusi pale huenda wasingetushika maskio kipindi cha utumwa…

Senior Answered on July 29, 2019.

Asante sana kaka

on July 31, 2019.
Add Comment

Sijawahi sikia kuwa shetani ni mweusi. Ila upande wa yesu ni sababu tumemfahamu kupitia biblia na biblia ndio imeonesha alizaliwa kipindi hicho hakukuwa na biashara ya utumwa hivyo. Ni uwezekano mdogo kwa eneo alilozaliwa (according to bible) yeye akawa mweusi. Kwani kipindi hicho kusafiri kulikuwa kuna mipaka ya bahari, tofauti na sasa.
Pili wa kuzaliwa na kufa kwa yesu ilikuwa bado mataifa yetu hayajui dini tofauti na mababu zetu. Tumeifahamu na kufahamu kuhusu dini ya kikristu miaka ya badae sana. Ila uwezekano wa kuwa ni mtu wa Uarabuni hii inawezekana.

Senior Answered on July 29, 2019.
Add Comment

Your Answer

By posting your answer, you agree to the privacy policy and terms of service.