Kwann michezo ya bahat nasibu na betting imekua na watumiaji wengi sana hasa katika nchi zinazoendelea..?

kwamba njia zingine za kujipatia ridhiki haziwanufaishi kadili ya mahitaj Yao?

Junior Asked on August 24, 2019 in Uchumi.
Add Comment
4 Answer(s)

Katika mataifa yanayoongoza kwa betying Africa hatupo, kutokana na kuchelewa kwa michezo hiyo ya bahati nasibu. Ila tangu kuja kwa michezo hiyo Africa ni moja ya sehemu zinakuwa kwa kasi. Mfano Naijeria hutumia zaidi ya $20 billion kwa mwaka, katika michezo ya bahati nasibu.

Sababu ya kukuwa kwa kasi katika mataifa yetu mimi naona ni kutokana na vijana kukosa ubunifu na juhudi katika kutafuta, hivyo wengi wanaamini betting ni mafanikio ya haraka, japo wengine ni bodaboda wakifanya shughuri zao wanapitia kubet.

Pia sababu nyingine ni kutokana na mtaji mdogo wa kubetia unaohitajika. Kuanzia jero 100, 200. Hivyo mtu au watu wanaona kupoteza kiasi kidogo kila siku sio shida.

Senior Answered on August 24, 2019.
Add Comment

Mataifa yanayoendelea watu wake wengi ni maskini na wanakipato kidogo sana na ndio maana zinapotokea fursa kama hizi za hela za kubahatisha , watu wengi hujitokeza kujaribu bahati zao kwani michezo hii huchezwa kwa pesa ndogo sana na matarajio ya kushinda pesa ndefu hivyo watu wengi huvutiwa ,,

Senior Answered on August 24, 2019.
Add Comment

Mi nadhani nchi zinaziendelea zimechelewa kabisa katika michezo hiyo ya kubahatish kw kuwa nchi tajir nyng tayari zilikuwa huko miaka na miaka. Kwa hiyo usidhani kuwa masikini ndio wachezaji wa michezo hiyo la hasha matajiri ndo wMebobea huko. 😜😜

Freshman Answered on August 24, 2019.
Add Comment

hii michezo ilikuwepo toka zamani sana ila kwa sasa wimbi limekua kubwa kutokana na vijana kua wengi sana na wengi kua hawana ajira au kipato chao hakutoshelezi hivo watu wanafanya kama chanzo chao rasmi cha mapato

Junior Answered on August 26, 2019.
Add Comment

Your Answer

By posting your answer, you agree to the privacy policy and terms of service.