Mambo gani ya kipekee kuhusu mwaka 2020 natakiwa niyajue?

Namini kila mwaka una sifa zake za kipekee, vipi kuhusu mwaka 2020?

Freshman Asked on December 4, 2019 in Swali la Kizushi.
Add Comment
1 Answer(s)

Mwaka 2020 utakuwa mwaka wa kipekee na muhimu sana katika kalenda ya maendeleo ya sayansi na teknolojia. Katika karne ya 20 mengi yalitabiriwa kuwepo au kufanyika katika mwaka 2020 ingawa baadhi tayari tumeyaona ‘mfano simu zilitabiriwa kuwa katikati ya maisha ya mwanadamu’.

Mwaka ambao nambari mbili za kwanza zinalingana na tarakimu mbili za mbele yake huja mara moja katika karne… kwa hivyo kuwa hai katika mwaka huo itakua kitu cha kipekee sana. Nna matabirio chanya juu ya mwaka huo ila kila nikiwaza mwaka 1919 (mwaka wa mwisho kufanana namba zake) nakumbuka mkataba wa amani wa Versailles uliosainiwa tarehe 28 juni mwaka huo.

Sophomore Answered on December 5, 2019.
Add Comment

Your Answer

By posting your answer, you agree to the privacy policy and terms of service.