Mwanamke ameshika mimba lakini bado anaendelea kupata mzunguko, shida nini?
Je sababu nini baadhi ya wanawake kuendelea kuingia kwenye siku zao hata wakiwa na mimba?
Spotting au kutokwa na damu kidogo ni wasiwasi wa kawaida ambao wanawake wengi wajawazito unawanakabili. Takriban 20% ya wanawake wanaripoti kuwa wanapata spotting (damu kidogo) katika wiki 12 za kwanza za uja uzito. Damu katika kipindi hicho cha ujauzito kawaida ni nyepesi kuliko wakati wa hedhi.
Ingawa ni rahisi kuhofia, usiogope. Hali ikizidi kuwa ya kutisha basi wahi kituo cha afya kwa msaada zaidi.