Ni kipi kinawafanya watu wengi wasiendelee?

Kwanini watu wengi hawaendelei

Junior Asked on July 30, 2019 in Ushauri.
Add Comment
1 Answer(s)

Kiuchumi watu wanafeli sana hapa bongo sababu kitu tunachoogopa ni kuchukua ‘risk’ na kukubali mabadiliko. Leo nikikwambia kuna biashara ambayo nataka tutumie ada yako na yangu then tufanye huo uwekezaji na baada ya mwaka, kuna uwezekano wa 80% kufanikiwa, na tukapata faida. Katika sentesi hiyo kitu ukicho notice ni neno UWEKANO. Ko hapo tayari ntapoteza watu 99% nitakao waambia hili wazo.

Katika upande wa mabadiliko nakupa mfano wa bongo movie na muziki. Katika bongo movie jamaa wamekataa kukubali kuwa hatuwataki sokoni na wakajiulize tunataka nini, ‘nobody want see their shit’ ambayo kila siku ni kuhusu love this and that, poor quality, hakuna investment katika research ya movie zao.

Katika bongo flavour bana mashabiki sisi tukiamka leo tunataka content za kijinga/matusi basi mwaka huu basi wasanii watafanya hivyo. Lakini kama wasanii wangedili kuandaa muziki mzuri na bora, bwana we utapata mashabiki tyu hata iweje. Eminem katika The Really slim shady alisema waandishi na mashabiki wanataka wampe Grammy ili wajisifu, yeye hataki tuzo hiyo. But Album hiyo ndio ilimpa Tunzo nyingi zaidi na ndio moja ya Album zake zilizosikilizwa sana. Ko i believe wasanii wakaamua kusimama katika ubora wa muziki, tungekuwepo hata kwenye #THEGIFT.

Pia kuna Mfumo wetu wa elimu. Sisi tz tangu nyerere hadi magu mfumo wetu hauna tofauti. Sidhani kama kuna mfumo wowte duniani ambao hauitaji mabadiliko ndani ya miaka 50. Hapo lazima watubwanaoendeshwa kwa mfumo huo wafeli. Lazima wafeli haina njia zaidi ya kubadiki mfumo. Nikupe mfano Singapore imetangaza kuanza kufundisha Coding kwa shule zote za msingi. Mimi na wtu wengine hapa bongo ambao hatusoma Computer katika level ya diploma, 99% hatujui coding lakini mtoto wa primary Singapore anajuwa. Unahisi kutakuwa na maendeleo kwa watu wengi kweli.

Mfumo wetubwa uchumi, Tanzania bana 77% wao kilimo ndio maisha yao, wakati USA 5% ndio wakulima, na katika hao 77% wengi wanalima kilimo cha mazao za kula like 80% , na pia ni 5% katika hiyo 77% wanalima kwa mvua. Hivyo mvua ikakataa basi 77% ya Watanzania watakufa njaa. Ko tungekuwa na diversification ya economy basi tungekuwa mbali saaaaana.

Senior Answered on July 31, 2019.
Add Comment

Your Answer

By posting your answer, you agree to the privacy policy and terms of service.