Ni mambo gani ya msingi unatakiwa kuangalia pale unapotaka kuelewa tabia za watu wanaokuzunguka?

Naomba msaada wa hili ili niweze kuamiliana/kuhusiana na watu vizuri.

Freshman Asked on August 15, 2019 in Uhusiano.
Add Comment
2 Answer(s)

1) Usijaribu kuhukumu tabia ya mtu bila kuelewa sababu zake za msingi
2) Namna mtu huonyesha tabia fulani katika hali tofauti itatoa kidokezo juu ya nia yake kuu.
3) Huwezi kuelewa tabia za watu kabla hujajua juu ya saikolojia yao. Nguvu fulani za kisaikolojia mara nyingi hujengeka kipindi mtu akiwa mtoto hivyo kama hujamjua tangu utotoni inakuwa shida, hivyo huna budi kuwa mtulivu maana taratibu utakuja jua ukweli wa mambo baada ya kukaa nae mda mrefu.

Sophomore Answered on August 15, 2019.
Add Comment
  • Jaribu kujielewa mwenyewe kwanza

hata kwa juu juu tu, inaweza kukusaidia kuelewa jinsi unavyofikiria na jinsi unavyoelewa wengine

 

  • Tambua aina tofauti za tabia.

Utaweza kuelewa watu vizuri ikiwa utathamini upeo na mtazamo wao.

 

  • Thamini utofauti

Badala ya kuhukumu, jaribu kukubali utofauti wa mtu. Itakua rahisi kumuelewa mtu endapo utakubali kuelewa kuwa sio lazima awaze kama wewe na wala usimlazimishe. Pia kujiweka katika viatu vya mtu mwingine kutasaidia kuto toa hukumu mapema.

Junior Answered on August 16, 2019.
Add Comment

Your Answer

By posting your answer, you agree to the privacy policy and terms of service.