Ni mwanasayansi gani aliyegundua bomu la nuclear na akajuta?

Answered

Ni mwanasayansi gani aliyegundua bomu la nuclear na akanuta?

Freshman Asked on January 15, 2020 in Technology.
Add Comment
1 Answer(s)
Best answer

Swali lako limenifanya nikumbuke kile nilichoambiwaga na wadau kuwa Albert Einstein ndiye aliyegundua bomu la nyuklia,ila sio kweli.

Einstein alihusika katika kuwaarifu wamarekani mwaka 1939 kuwa wamarekani wanatakiwa waanze utafiti wa kuunda bomu la atomiki kwa kuwa ilihisiwa kuwa wajerumani chini ya Hitler walikuwa na Uranium, hiyvo inahitajika Marekani waharakishe kutengemeza bomu hilo. Hapo tena yakaanza mashindano ya nani atafaulu kwanza kulifikia lengo hilo.

Kumbuka kipindi hicho manuwari za Wamarekani zilishambuliwa na ndege za Wajapani huko Pearl Harbor, Honolulu, Hawaii. Hivyo, ililazimu kujengwa maabara ya utafiti wa atomiki kwa haraka kama iwezekanavyo, na ndipo Los Alamos pakachaguliwa kuwa ni mahala muwafaka pa kufanya jaribio hilo, na mradi huo ukapewa jina la Manhattan na Mwanafizikia Robert Oppenheimer aliiongoza shughuli hiyo katika kipindi cha chini ya miaka miwili

Mgunduzi wa bomu la nyuklia,Robert OppenheimerMgunduzi wa bomu la nyuklia,Robert Oppenheimer

Wengi wa wanasayansi walioshiriki katika mradi huo walidhani kwamba habari za kufaulu majaribio ya kuripuwa bomu la kinyukliya yataifanywa Japan ivikomeshe Vita Vikuu vya Pili vya Dunia. Lakini Rais Truman wa Marekani na wanajeshi wake waliamuwa vingine. Wiki tatu baadae mabomu ya atomiki yalidondoshwa huko Hiroshima na Nagasaki Agosti mwaka 1945 na kupoteza maisha ya watu 130,000, wengi wao wakiwa ni raia. Nguvu kubwa ya uharibifu wa bomu hilo ilimshangaza pia mvumbuzi wake, Robert Oppenheimer, na kumweka katika hali ya wasiwasi.

Sophomore Answered on January 16, 2020.
Add Comment

Your Answer

By posting your answer, you agree to the privacy policy and terms of service.