Nini maana ya “muda”?

Muda

Freshman Asked on August 22, 2019 in Historia.
Add Comment
1 Answer(s)

Muda (Time) ni dhana ambayo imejadiliwa sana na watu katika kuutafuta ukweli wake, Muda wengine wanaita Wakati, wengine wanaita Majira, wengine wanaita masaa au zama. Walijitokeza wasomi, wanafalsafa na wanasayansi wakubwa na maaarufu ambao nao kwa nafasi zao walijaribu kutoka majibu ya swali hili “MUDA NI NINI?” “WHAT IS TIME?”

Katika mijadala yao yalijitokeza makundi matatu yaliyokua na mitazamo inayopingana kuhusu muda. Kundi la KWANZA likiongozwa na mwanasayansi maarufu SIR ISAAC NEWTON, walidai kuwa muda ni kitu kinachojitegemea na ni sehemu ya umbo la ulimwengu ambalo ndani yake ndimo matukio mbalimbali hutokea, kwa maana nyingine ni kwamba Newton alisema Matukio yanatokea katika msatari wa muda ambao tayari upo. Nadharia zenye mtazamo wa kundi hili tunawaita NEWTONIAN TIME.

Kundi la PILI, kundi hili linaongozwa vile vile na mwanasayansi maarufu ALBERT EINSTEIN. katika kitabu chake maarufu kilichopata kuuzika sana kinachoitwa THE SECRET(2014), Einstein alisema, “Time is just an Illusion” (katika tafsiri isiyo rasmi, alimaanisha kwamba “Muda ni mawazo tu au mauzauza au fikra tulizozijenga akilini mwetu ambazo hazina ukweli wowote”).

Wananadharia wa kundi hili wanasema kuwa, muda hauna uhusiano wowote na matukio, wala hauna uhusinao wowote na huo mstari ambao matukio yanaufuata ili yatokee, bali muda ni dhana tu ya kisomi iliyobuniwa inayotumika kuelezea mpishano wa matukio. Yaani muda ni dhana tu akilini mwetu, kusipokuwepo kitendo muda hauwezi kuwepo.

Waliongeza kwa kusema kwamba, Muda hupimwa kwenye nafasi(space) ambamo ndimo matukio hutokea. Matukio au vitendo hivyo ni kama vile, Usiku au Mchana, asubuhi, jioni, kuzaliwa – ukuaji – kuzeeka – mapaka kifo.

Hivyo wanasisitiza kwamba Muda hauishi sehemu yoyote na hauwezi kujitegemea.

Kundi la TATU, hawa ni wananadharia waliokuja na wazo linalopingana na makundi yote hayo matatu yaliyotangulia, wao walisema “Muda si kitu cha kweli/Halisi kinachoweza kujitegemea kama madai ya Newtonian Time yalivyosema wala muda si Mawazo au jambo lililobuniwa akilini mwa mwatu kama mawazo ya Einstein na wenzake yaliyodai”. Bali wao walisema “Muda ni UBUNIFU na KUMBUKUMBU tu za mwanadamu zinazomsaidia kuyafanya mambo yawe ukweli”.

Mmoja wa wananadharia wa mlengo huu MARTIN HEIDEGGER anaamini kwamba Hatuishi ndani ya muda, sisi wenyewe ndio Muda. Hivyo, uhusiano tulionao juu ya wakati uliopita(Past Experience) ni ufahamu wa wakati uliopo(present awareness) katika mambo yaliyopita, Ufahamu huo unaturuhusu kuufanya wakati uliopita uweze kuishi ndani ya wakati uliopo. Uhusinao tulionao kwa wakati ujao (future) ni makisio ya uwezekano fulani, kazi au maungano ya vitu, ni jambo linalotafsiri hali ya mtu kujali kitu au uhusika wake wa moja kwa moja na kitu hicho, kitendo kinachomfanya awe mbele ya mahala alipo sasa (being ahead of oneself) pale anapowaza mambo ambayo hayajatokea (pending occurance). Hivyo basi wanaona kua ile hali ya mtu kujali uwezekano wa mambo Fulani kuweza kutokea vile vile kunaruhusu wakati ujao kuweza kuishi ndani ya wakati uliopo.

Senior Answered on August 22, 2019.
Add Comment

Your Answer

By posting your answer, you agree to the privacy policy and terms of service.