Sina ufahamu wowote kuhusu upigaji picha,Nifanyaje na niwe na vifaa gani ili niwe Mpiga picha bora?

swali langu ni kuwa na hitaji kuwa MPIGA PICHA na sina ufahamu wowote kuhusu nadharia hiyo ni fanyaje na mtu unatakiwa  na uwe na vifaa gani ili niwe  MPIGA PICHA MZURI NA BORA

Freshman Asked on October 1, 2019 in biashara.
Add Comment
2 Answer(s)

Nakupa hongera kwa kutambua ‘hobi’ yako. Upigaji picha ni fani ambayo ilikuwa kazi kwangu tangu mwaka 2016 mpaka 2018. Kabla ya kuingia katika fani hiyo nilikuwa nasita sana kuifanya kazi kwa kuwa nilikuwa nna kamera ndogo ya powershot sx 40 ambayo kibiashara kwa sasa haikufaa, yaani iphone 7 ilikuwa inatoa picha nzuri kuishinda. Lakini rafiki yangu mmoja wa karibu Musa Malangalila alinifundisha kitu muhimu sana katika fani hii. Huyu jamaa alikuwa akishika kamera yangu ambayo nilikuwa nikiidharau basi picha ikitoka ni lazima uwe bomba na sio siri watu wengi hawakupenda niwapige picha kwa kuwa walijua utaalamu aliokuwa nao rafiki yangu.

Kwanini nimekupa kisa hiko? nataka utambue kuwa, ubora wa vifaa sio kitu katika fani inayohusisha ubunifu. Kwa taarifa yako, njia pekee ya kuwa mtaalamu wa kupiga picha ni kujinoa zaidi kimafunzo tena kwa ulimwengu wa sasa wa .com kila kitu utapata mtandaoni mfano YouTube

Tafuta wapiga picha bora unaowajua kuwa nao karibu hata kuwa’follow’ katika mitandao ya kijamii kwa kufanya hivyo itkuongezea hamasa ya kuzidi kuipenda fani hiyo. Asante

Professional Answered on October 1, 2019.
Add Comment

Sawa nimekuelewa ila waweza nitajia hao wapiga picha zenye ubora kusudi niwe karbu nao nisaidie tafadhali nahitaji kweli

Freshman Answered on October 3, 2019.
Add Comment

Your Answer

By posting your answer, you agree to the privacy policy and terms of service.