Kidato cha nne nimepata division 2, Nikasomee kozi gani kuhusu kompyuta?

Nimemaliza form 4 nikiwa na division 2 ya 21 combinations zote zimebalance isipokuwa combinations zenye physics kwani physics Nina F.sitaki kusoma A-level nataka kwenda chuo moja kwa moja.Ni kozi gani nikasome huko chuo inayohusiana na computer.Tayari mkononi ninajua VFX vizuri nilijifunza mwenyewe sasa naona kama nyota yangu ipo kwenye computer.Ni Kozi gani nikasome uko chuo naombeni ushauri wadau wa swahiliqa

Freshman Asked on January 10, 2020 in Ushauri.
Add Comment
2 Answer(s)

Naona,Telecommunication na Computer science ila wewe unataka nini? jiulize hilo swali kwanza

Sophomore Answered on January 13, 2020.
Add Comment

Swali lako zuri sana na inaonekana kwa namna fulani tunalandana..Binafsi ninafanya kila kitu pia katika graphics (photoshop, illustrator, After effects na premiere pro)  hadi animations,na kuhusu VFX ndio usiongee kabisa. Nilipomaliza form 4 niliigia katika uzalishaji wa filamu na kwa mara ya kwanza nilishuti na kuedit filamu iitwayo “Kisasi” hadi kufikia form 6 nikawa nimeshuti filamu tatu jumla.

Lakini tofauti na wewe nilipomaliza form 6 sikutamani kabisa kusomea editing wala web development, nilichokifanya nikaenda chuo Kikuu cha Dar es salaam kusomea Marketing lakini kutokana na sababu fulani chuo niliacha. Taratibu nkajiendeleza katika ujuzi wangu wa graphics na mwishowe nikajikuta naingia katika web development, ingawa sio fundi sana katika web lakini kwa ujuzi mdogo nilionao nimefanikiwa kufanya mambo mengi katika uwanja huu na leo hii nikishirikiana na wenzangu tumekuja na website hii ya SwahiliQA ya maswali na majibu ya kiswahili. Sasa, kitu muhimu ni nini? usisubiri chuo ndo ujue utaenda kusomea nini…anza sasa, kaam unapenda kompyuta we anza tuu fanya usisubiri mwalimu. Asante

Ukitaka kuona baadhi ya kazi zangu az graphics bonyeza link hii

Professional Answered on January 14, 2020.
Add Comment

Your Answer

By posting your answer, you agree to the privacy policy and terms of service.